TanzaniaEntertainment

G Nako Atangaza Kuja Kwa EP Mpya ‘Yellow Tapes’

Featured in this story

Rapper maarufu wa Tanzania, G Nako, amewatangazia rasmi mashabiki zake kuwa yuko tayari kuachia EP yake mpya inayoitwa Yellow Tapes, inayokuja hivi karibuni.

Katika video fupi aliyoweka Instagram, G Nako amejionyesha katika mtindo wa picha ya mugshot ya kifungo, akiwa amevalia suti ya mistari, kofia, miwani meusi na meno ya dhahabu. Akishika kibao cheusi kilichoandikwa “G NAKO | YELLOW TAPES” kwa herufi za manjano.

G Nako aliandika kwenye chapisho lake: “NAPENDA KUWATANGAZIA KUWA MY NEW EP IPO NJIANI #YELLOWTAPES,” na hivyo kuzua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa hip hop na Bongo Flava.

Yellow Tapes inatarajiwa kuwa moja ya project itakayoleta mvuto mkubwa katika tasnia ya muziki wa hip hop nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka huu. Tarehe rasmi ya kuachia bado haijatangazwa, lakini G Nako amedokeza kuwa EP hiyo iko njiani.

New
Browse
t tt tt t t t tt tt
Explore
Shorts
Artists