Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kupitia akaunti ya mtandao wa Instagram @basata.tanzania limetangaza kuwa zoezi la utolewaji wa Tuzo za muziki Tanzania (TMA 2024) utafanyika usiku wa tarehe 19 Oktoba mwaka huu.

Mchakato wa tuzo hizo ulianza machi mwaka huu 2024 huku nominations zake zikitangazwa Agosti 29 mwaka huu na upigaji wa kura ulizunduliwa rasmi September 3.
Kamati kuu inayoratibu na kusimamia tuzo hizo ikiongozwa na Seven Mosha imeahidi kufanya makubwa na kuonyesha utofauti wa kipekee kwenye tuzo hizo mwaka huu tofauti na miaka mingine.