Entertainment

Jiandae na ROOM NUMBER 3 EP Kutoka Kwa Mbosso

Jiandae na ROOM NUMBER 3 EP Kutoka Kwa Mbosso

Dar es Salaam, Tanzania – Habari njema kwa mashabiki wa Bongo Flava! Msanii nyota Mbosso amethibitisha kuwa Extended Play (EP) yake mpya, “ROOM NUMBER 3,” inatarajiwa kuachiwa rasmi kesho, Juni 12, 2025, kwenye majukwaa yote ya muziki ya kidijitali.

Ingawa orodha kamili ya nyimbo na wasanii walioshirikishwa bado haijatangazwa, Mbosso amewapa nafasi mashabiki wake waanze kuipata EP hiyo mapema kwa kuweka pre-order kuanzia sasa. Hii inawapa fursa ya kuwa wa kwanza kuisikiliza mara tu itakapowekwa hewani.

Jiandae na ROOM NUMBER 3 EP Kutoka Kwa Mbosso
Jiandae na ROOM NUMBER 3 EP Kutoka Kwa Mbosso

“ROOM NUMBER 3” inafuatia kipindi cha kimya cha takriban miezi minne kutoka kwa Mbosso, na inaashiria kazi yake ya kwanza tangu atangaze kuondoka Wasafi Classic Baby (WCB) mwezi Februari, 2025. EP hii inatarajiwa kuonyesha upande mwingine wa Mbosso, huku akiahidi muziki wenye hisia na ujumbe mzito kama ilivyo ada yake.

Hakikisha unajiandaa kuipokea kazi hii mpya kutoka kwa Mbosso na Konde Music Worldwide! Je, unadhani ni nyimbo gani zitakuwa kali zaidi kwenye EP hii?

New
Browse
Explore
Genre
Artists