Dar es Salaam, Januari 2025 – Msanii wa Hip Hop wa Bongo Flava, Darassa, amewapa mashabiki wake zawadi ya mwaka mpya kwa kutangaza ujio wa albamu yake mpya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa alituma salamu za heri ya mwaka mpya kwa mashabiki wake na kisha kutangaza habari njema kuhusu albamu yake. “2025 GODSPEED, CMG FOR LIFE, ALBUM YA #MRBURUDANI INAKUJA THIS JANUARY IN SHA ALLAH 🙏🏽,” aliandika katika maelezo ya video yake.
Ingawa jina rasmi la albamu hiyo halijatangazwa, hii itakuwa albamu ya pili ya Darassa tangu atoe albamu yake ya kwanza, “Slave Becomes A King,” mwaka 2020. Mashabiki wanaweza kutarajia kusikia muziki mpya kutoka kwa msanii huyo mahiri hivi karibuni.